Rais wa Ukrain Aiomba Nato Kutumia Meli

Rais wa Ukrain Aiomba Nato Kutumia Meli
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko ameiomba Nato kutuma meli kwenda bahari ya Azov kufuatia makabiliano yaliyotokea kati ya Ukraine na Urusi baharini eneo la Crimea.

Poroshenko aliliambia gazeti la Ujerumani Bild kuwa anaamini kuwa meli hizo zitapelekwa "kuisaidia Ukraine na kuweka ulinzi".

Siku ya Jumapili Urusi ilivamia meli tatu za Ukraine na kuwashika mabaharia wake kutoka Kerch strait.

Nato imesema inaunga mkono Ukraine ambayo si mwanachama wake.

Siku wa Jumatano Rais wa Urusi Vladimir Putin alimlaumu Bw Poroshenko kwa kuanzisha uhasama wa baharini ili kujiongeze umaarufu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2019.

'Sipendi uchokozi' kauli ya Trump kwa Urusi
Rais Poroshenko alitanga sheria ya kijeshi sehemu za mpaka wa Ukraine kwa siku 30 kama jibu kwa mzozo huo.

Wakati wa mahojiano na Bild, Bw Poroshenko alisema Vladimir Putin alikuwa na mpango wa kudhibiti bahari ya Azov.

"Ujerumani ni mmoja wa washirika wetu wa karibu sana na tunamatumaini kuwa nchi kwenye Jumuiya ya Nato sasa ziko tayari kupeleka meli katika bahari ya Azov ilia kuisaidia Ukraine kuweka ulinzi," alisema.



"Hatuwezi kukubali sheria hii ya uchokozi ya Urusi. Kwanza ilikuwa ni Crimea, kisha mashariki mwa Ukraine, na sasa anataka bahari ya Azov. Ujerumani pia inastahili kujiuliza: Ni kipi tena Putin atafanya kama hatuwezi kumzuia?"

Siku ya Jumatatu, mkuu wa Nato Jens Stoltenberg alitoa wito kwa Urusi kuziachilia meli za Ukraine na kusema ni lazima Urusi ijue kuwa kuna madhara kwa vitendo vyake.

Alisema kuwa Nato itandelea kutoa msaada kwa Ukraine ambayo ni mshirika wa Nato, ingawa si mwanachama kamili.

Je sheria ya Kijeshi itatumika Ukraine baada Urusi kuziteka meli zake?
Nato haikujibu mara moja taarifa za hivi punde kutoka kwa Bw Poroshenko.

Kipi kilifanyika huko Crimea?
Takriban wanajeshi watatu wa Ukraine walijeruhiwa wakati walinzi wa mpaka wa Urusi walifyatulia risasi boti mbili za kivita za Ukraine na boti nyingine ndogo karibu na Crimea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad