Rais wa Uturuki: Amri ya Kumuua Khashoggi Ilitolewa na Viongozi wa Ngazi za Juu Saudia

Rais wa Uturuki: Amri ya Kumuua Khashoggi Ilitolewa na Viongozi wa Ngazi za Juu Saudia
Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoÄŸan amesema kuwa amri ya kumuua mwandishi wa habari Jamal Kashoggi ilitolewa na viongozi wa ngazi za juu kabisa katika serikali ya Saudi Arabia.

"Amri ya kumuua Khashoggi ilitolewa na viongozi wa ngazi za juu Saudia"
Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoÄŸan amesema kuwa amri ya kumuua mwandishi wa habari Jamal Kashoggi ilitolewa na viongozi wa ngazi za juu kabisa katika serikali ya Saudi Arabia.

Katika makala iliyoandikwa na "Washington Post",rais ErdoÄŸan amesema kuwa ana uhakika kuwa wahuiska ni kati ya washutumiwa 18 waliokamtwa nchini Saudi Arabia.

"Tunajua kuwa wauaji walitumwa kuja Uturuki na kummaliza Khashoggi baada ya hapo walifunga safari na kuondoka na amri hiyo ilitolewa na serikali ya Saudi Arabia",alisema ErdoÄŸan.

Khashoggi alipotea 2 Oktoba baada ya kuingia ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul.

Kulingana na ripoti iliyotolewa nchini Uturuki,mwandishi huyo alinyongwa mara tu  alivyoingia katika  na kisha mwili wake kukatwakatwa.

Rais  ErdoÄŸan anaamini kuwa mauji hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kitambo.

Rais wa Uturuki amedai kuwa kuna maswali mengi ambayo mpaka hivi sasa hayajajibiwa na serikali ya Saudi Arabia na yanabaki kuwa ni fumbo.

"Khashoggi ana haki ya kuzikwa katika misingi ya dini ya kiislamu na ni jukumu letu kuhakikisha ndugu na jamaa wa marehemu wanamuaga mpendwa wao kwa heshma zote",aliongeza ErdoÄŸan.

ErdoÄŸan amesisitiza kuwa mauaji hayo hayakuamrishwa na mfalme wa Saudi Arabia,Salman.

Mahusiano mazuri ya muda mrefu kati ya Saudi Arabia na Uturuki hayataizuia Ankara kuchukua hatua dhidi ya mauaji ya kinyama ya  mwandishi Jamal Khashoggi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad