Rais wa TFF Amkingia Kifua Amunike Awaonya Mashabiki na Wadau wa Soka

Kaira Amkingia Kifua Amunike Awaonya Mashabiki a Wadau was Soka
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia, amewataka mashabiki na wadau wa mpira wa miguu nchini kuacha kuingilia majukumu ya Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike.

Karia amevunja ukimya kwa kusema Amunike anapaswa kuheshimiwa juu ya taaluma yake hivyo ni vema akaachwa ili atimize wajibu wake.

Hayo yamekuja kufuatia Kocha Amunike kuanza kutupiwa vijembe na hata lugha isiyo rafiki baada ya Taifa Stars kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019 huko Cameroon.

Rais amefunguka hayo kutokana na Amunike kushutumiwa jambo ambalo anaamini ni kuingiliwa kwa taaluma ya kocha huyo ambaye aliwahi kusakata kambumbu la kimataifa.

Sanjari na hayo, Amunike amewataka mashabiki wa soka nchini kuwa na uvumulivu kwani Stars itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Uganda ambao ana imani timu itafanya maajabu na kufuzu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad