Rapper Fid Q Afunguka Mpaka wa Kuoa December


Rapper Fid Q ameweka wazi kuwa mwaka huu mwezi Desemba Mungu akipenda na yeye anafunga ndoa, hii ni baada ya kuvutiwa na maisha mapya ya Stamina na mkewe.


Fid Q amesema hayo Wiki iliyopita kwenye sherehe fupi ya kumbu kumbu ya siku ya kuzaliwa Stamina, ambapo alieleza kuwa maisha ya ndoa yanambadilisha mtu.

“Kitu ambacho hukifahamu wewe (STAMINA) au labda watu wengi hawakifahamu. Wewe pia unani-inspire mimi siku hizi unanielewa vizuri, Unani-inspire kama Artist, Lifestyle, umebadilika sana siku hizi umekuwa mtu wa familia.  Kwa kupitia wewe mimi nina mpango wa kuoa mwezi Desemba,“amefunguka Fid Q.

Fid Q kwa sasa ana watoto, lakini hajafanikiwa kufunga ndoa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad