Msanii wa muziki Rayvanny bado hajaondoa wimbo ‘Mwanza’ mtandaoni kama alivyoagizwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa madai wimbo huo hauendani na maadili ya Kitanzania.
Rayvanny kupitia waraka huu hapa chini ameeleza sababu za kuandaa wimbo huo huku akikosoa mambo mengi yaliyoelezwa na baraza hilo.
Part 1; HABARI ZA ASUBUHI NDUGU ZANGU…….
TAARIFA ZA KUFUNGIWA KWA WIMBO WANGU NIMEZIPATA…..
LAKINI KATIKA HILI NINA HAYA MACHACHE YAKUSEMA…… ..1.SANAA NI NINI??? ….SANAA NI NENO LILILOTOKANA NA LUGHA YA KIARABU…. LENYE MAANA NI UFUNDI ANAOUTUMIA MWANADAMU, KUWASILISHA FIKRA AU MAWAZO YALIYO NDANI YA FIKRA ZAKE…..VILE VILE SANAA NI UZURI UNAOJIIBUA KATIKA UMBO #LILILOSANIFIWA…. #KUSANIFU NI KUUMBA/KUFANYA KITU KWA KUTUMIA USTADI ILI KIWEZE KUVUTIA WATU KWA UZURI WAKE…. HIVYO KAZI YOYOTE YA SANAA INATEGEMEA IONYESHE UFUNDI WA HALI YA JUU, ILI IWE NA MVUTO KWA HADHIRA YAKE #ILIOKUSUDIWA………… HAYO MANENO SI YANGU MIMI NI TAFSIRI YA NENO SANAA………. .
….2.DHAMIRA YA WIMBO……..
.DHAMIRA YETU HAIKUA KUTUKANA, KAMA INAVYOONEKANA SASA… DHAMIRA YETU ILIKUA KUTOA BURUDANI KWA HADHIRA ILIOKUSUDIWA AMBAO NI VIJANA WENZETU LAKINI PIA NA MAFUNDIOSHO AMBAYO KILA SIKU SERIKALI IMEKUA IKIYAPIGA VITA……
SWALA KAMA LA AMBEL RUTI…. KATIKA WIMBO WETU TUMESEMA…. (NAMI NAOGOPA SENTRO MICHEZO YA AMBEL RUTI, KWAMBA KIJANA YOYOTE ANAESIKILIZA AOGOPE KITENDO HICHO ATAISHIA PABAYA……..
PIA KUNA MISTARI INASEMA…. (HAPENDAGI MPASUO….ATAKI SHIDA BASATA) UKIWA NA MAANA YA KUKATAZA MAVAZI MABAYA/ MAVAZI YA WAZI NAKUSISITIZIA KWAMBA HATA BASATA HAYARUHUSIWI….. UKIANGALIA HAYA YOTE NI MAFUNDISHO AMBAYO MWANASANAA LAZIMA UYAFIKISHE KATIKA LIGHA ILIOSANIFIWA………..3.KWANINI MWANZA…….TUNGEWEZA KUUITA HUU WIMBO JINA LINGINE LOLOTE , MBEYA ,KIGOMA AU MKOA WOWOTE TOFAUTI LAKINI KWANINI #MWANZA…… IKUMBUKWE SIKU CHACHE ZILIZOPITA KUMETOKEA MAAFA MAKUBWA YALIYOWAKUTA NDUGU ZETU WA MWANZA…. WATU WAMEPOTEZA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI…..KAMA WASANII TULIWAZA SANA HUSUSANI KWA VIJANA WENZETU WA MWANZA TUWAFANYIE KITU GANI IKIWA NI SEHEMU YA FARAJA KWAO….. NDIPO LILIPOKUJA WAZO LA KUTENGENEZA WIMBO KWA AJILI YA #MWANZA……. UNAOSEMA KWETU MWANZA #NYEGEZI LAKINI TUKASEMA USIENDE HIVYO TU UWE NA MAFUNDISHO NDANI YAKE LAKINI PIA BURUDANI KWA VIJANA WA MWANZA NA MAENEO MENGINE….NA KIUKWELI WIMBO HUU UMEPOKELEWA VIZURI SANA MWANZA NA MAENEO MBALIMBALI IKIWA NI ISHARA YA ILE DHAMIRA TULIO IKUSUDIA IMEFANYA KAZI…….
PART 2……. 1.KUFUNGIWA…….. KUNA VYOMBO VYA HABARI…NA SEHEMU MBALI MBALI MIZIKI YETU INAPOSIKIKA YAWEZEKANA KUKAWA NA WATOTO PENGINE WIMBO HUU HAIKUA NI HADHIRA TULIOIKUSUDIA….. HIVYO UKISIKIKA KWAO IKAWA NI KINYUME NA MAADILI KWA SABABU HADHIRA TULIOIKUSUDIA NI YA WATU WAZIMA YANI MIAKA 18 NA KUENDELEA…
AMBAO TUNAAMINI NDIO WAPO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII…NA NDIO WANUNUZI WA KAZI ZETU….NA NDIO WAHUDHULIAJI WA MATAMASHA YETU…….. 2..MAONI YANGU…….. NILIKUA NAONA SWALA LA KUFUNGIA WIMBO HUU KWA VIJANA WENZETU NI KUTUNYIMA KUFIKISHA UJUMBE…BURUDANI KWA HADHIRA YETU YA SANAA…..MFANO… MITANDAO YA KIJAMII, HAKUNA MTOTO ATAKE INGIA KATIKA MITANDAO….LAKINI PIA KWENYE MATAMASHA KAMA WASAFI FESTIVAL PALE WANAOKUJA NI WATU WAZIMA….AMBAO WIMBO HUU HAUNA MADHARA KWAO…… KWENYE TV NA REDIO NAWEZA KUSEMA NI SAWA KUTOKANA NA WATOTO WATAKAO TAZAMA WIMBO HUU ILA MITANDAO YA KIJAMII NA KWENYE MATAMASHA NAOMBA BARAZA LA SANAA TANZANIA (BASATA) MKIWA KAMA WALEZI WASANII MULITAZAME HILI NA KUONA MNATUSAIDIAJE….. SANAA NI KAZI / SANAA NI AJIRA LAKINI PIA SANAA NI UBUNIFU ASANTE…….