RC Mwanri Aagiza Bodaboda Kununua Pafyumu

RC Mwanri Aagiza Bodaboda Kununua Pafyumu
Mkoa wa Tabora umejipanga kutoa huduma za uhakika pamoja na usalama katika kipindi cha siku tatu kuanzia leo Jumatano wakati wa jukwaa la fursa za uwekezaji na biashara linalotarajiwa kufunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza mjini Tabora Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri amewahakikishia wageni zaidi ya 500 watakaohudhuria watakuwa salama na kupewa huduma iliyo bora, na kusema tayari wamezungumza na watoa huduma ya usafiri wa bodaboda kuwa waaminifu kwa wateja wao pale watakaposahau mali zao.

"Kwa wale watakaosahau mkoba kwenye bodaboda watajikuta wanapelekewa mikoba yao na waendesha bodaboda kwani hivyo ndivyo tulivyojipanga, pia nimezungumza na waendesha bodaboda kununua pafyumu kila mtu ili wateja wao washangae na kutoisahau Tabora" amesema Mwanri.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka wananchi na wajasiriamali kuitumia fursa hiyo kikamilifu kujiongezea kipato ili kupambana na umaskini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad