RC Simiyu, Anthony Mtaka Aonyesha Ndio RC Bora Kwa Vitendo "Sitoruhusu ‘Nguvu ya Polisi' Kwenye Uongozi Wangu"

Nilipata muda wa kufuatilia mahojiano ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, ndugu Anthony Mtaka kupitia televisheni ya taifa, TBC1.

Alizungumza mengi, ila binafsi nilivutiwa zaidi na haya yafuatayo;

1. Police economy
RC Mtaka anasema katika uongozi wake asingependa kutumia amri za kipolisi katika kuendesha uchumi wa Simiyu. Anasema kazi ya Polisi ni kulinda raia na mali zao, hivyo kama atalazimika kuwatumia Polisi kwenye masuala ya uchumi, basi ni kuwaagiza wahakikishe wafanyabiashara wanafanya kazi muda wote kwa usalama.

2. Muda wa Biashara
Anaamini ili kuchochea ukuaji wa uchumi, ni vyema biashara zikafanyika nyakati zote; usiku na mchana , badala ya kupangia watu muda wa kufanya biashara kana kwamba wateja wote wana ratiba zinazofanana.

Mathalani, anashangaa inakuwaje Bar zinapangiwa muda wa kufungua na kufunga wakati wanywaji wa bia ni watu wenye shughuli tofauti na wanaoingia makazini kwa nyakati zisizofanana? Wale wanaoingia shift za jioni/usiku, mchana wasinywe bia?

Aidha, anasema nchi kama Kenya pale Nairobi ukienda Airport usiku ni kama mchana, watu wako bize na biashara muda wote. Tofauti na Dar au KIA ambapo ukiwa Airport usiku huwezi kupata hata usafiri tu kwa haraka.

Akahoji pia zile taa za barabarani zipo kwa ajili ya ulinzi na watu kuweza kufanya biashara kama ilivyo mchana. Sasa kwanini usiku biashara zifungwe mapema hasa kwenye Miji ya biashara? Shida iko wapi? Maono.

3. Ushindani
RC Mtaka anashangaa Tanzania tunashindana na nchi gani kiuchumi? Kwa sababu nchi zinazoizunguka Tanzania zina mentality ya kufanya kazi kama mchwa tofauti na hapa. Anaamini bado kuna watumishi hawajaamka na kujua dhamira ya Rais Magufuli kuhusu uchapaji kazi. Anasema ataonesha mfano kupitia Simiyu na ndani ya miaka 3 ata-prove anayoyasema.

4. Wananchi
Kwa nilivyomuelewa, RC huyu anafikiria wananchi ni sehemu muhimu katika kukuza uchumi halisi kwa haraka. Anasema wananchi wengi wanaishi kwa mazoea na wanahitaji kuzinduliwa fikra zao tu ili watumie kwa ushahihi rasilimali walizonazo kujineemesha.

Anasema yeye binafsi amekuwa akiwahimiza wana-Simiyu kubadili mtindo wa maisha na wajiongeze ili kuweza kuishi maisha tofauti na sasa. Mfano, wafugaji wenye mifugo lukuki aliwashauri wakubali kuuza sehemu ya mifugo yao na kutumia pesa kufanya maendeleo binafsi na kweli wapo waliofanikiwa sana mpaka kujenga hoteli na kufungua miradi iliyowakomboa kimaisha.

Ukimsikiliza anavyozungumza na mambo anayoyafanya mkoani Simiyu, unaona kabisa ni kiongozi anayesoma, ana exposure, yuko serious na anayejua kuweka mipango inayotekelezeka. Sio mtu wa porojo za kisiasa.

Mambo ni mengi, ila kimsingi RC huyu ni hazina. Anataka kama nchi ina dhamira ya kukua kiuchumi kweli, basi ni lazima watu wabadili mtazamo na waige mtindo wa kufanya mambo kutoka kwa nchi zilizofanikiwa ili angalau nchi iingie kwenye ushindani.

Nimekumbuka: Hivi Rais Magufuli si alisema kwa mujibu wa ripoti alizonazo, zinaonesha RC Mtaka ndiye RC anayeongoza kwa kufanya kazi nzuri kuliko RCs wote nchini?

Haishangazi!

By Travic
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad