Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 na mchumba wake aliyemvisha Pete ya uchumba siku kadhaa zilizopita Georgina Rodriguez walionekana wakitembelea kanisa la Gran Madre di Dio lililopo jijini Turin, Italia
Mchezaji huyo machachari ameonekana kuwa na furaha na familia yake licha ya kukumbwa na kashfa ya kubaka huko nchini Marekani.
Taarifa za mtandao wa Daily Mail, zinadai huwenda wawili wao wakafunga ndoa ya kifahari nchini humo kabla ya mwaka huu haujamalizika.