Ushindi wa jana wa Manchester United dhidi ya Juventus haukustahili, kulingana na kauli ya nyota wa Kireno, Cristiano Ronaldo.
Cristiano Ronaldo anasema Manchester United "haikufanya chochote kustahili kushinda mchezo huo" baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya usiku wa Jumatano.
Nyota huyo wa Kireno alifungua kalamu ya mabao katika mchezo huo kwa kuifunga timu yake ya zamani kwa mpira wa 'volley' katika dakika ya 65, lakini mchezaji Juan Mata alisawazisha katika dakika ya 86, kabla ya Alex Sandro kujifunga dakika tatu baadaye na kuifanya United kuondoka na ushindi.
Ronaldo hakuvutiwa na staili ya uchezaji ya Man United, hata hivyo, anaamini Juventus ilitakiwa kuweka hesabu zake vizuri kwa kupata magoli dakika za mwanzo kabla ya hata ya mabao hayo ya kushtukiza ya United.
"Sisi tuliiongoza mchezo kwa dakika 90, tulikuwa na nafasi nyingi, tungeweza kuwaua mara tatu au nne, lakini tulifurahia mchezo na tukaadhibiwa," amesema Ronaldo.
"Manchester United haijafanya chochote kushinda mchezo. Huwezi hata kuzungumza juu ya bahati, kwa sababu unapaswa kuitafuta bahati yako na katika kesi hii tuliwapa tu. Sasa tunapaswa kuinua vichwa vyetu, kama tulicheza vizuri na bado ni juu ya kikundi," ameongeza.
Juventus bado ipo juu ya kundi H, ikiwa na pointi tisa, mbili mbele ya Manchester United ambayo ipo katika nafasi ya pili