Mchezaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuisadia timu yake ya Juventus kuondoka na ushindi wa goli 2-0 katika uwanja wa Sansiro
Ronaldo alifunga goli la pili mnamo dakika ya 81 baada ya Mario Mandzukic kufunga goli la mapema mnamo dakika ya 8 tu ya mchezo, baada ya matokeo haya yanaifanya Juventus kujikita kileleni kwa kuwa na alama 34 wakicheza michezo 12 wakishinda michezo 11 sare 1 na wakiwa hawajapoteza mchezo wowote. Napoli wakishikilia nafasi ya pili wakiwa na alama 28 huku AC Milan wakiwa katika nafasi ya 5 na alama 21.
Ikumbukwe kuwa Juventus walipoteza mchezo wao wa kwanza tangu msimu huu uanze wakipigwa goli 2-1 na Manchester United katika michuano ya UEFA wakiwa nyumbani na goli pekee la Juventus lilifungwa na Ronaldo.
Katika mchezo huu wa Juventus dhidi ya AC Milan ilikuwa ni siku mbaya kwa Gonzalo Higuain dhidi ya timu yake ya zamani, Lakini ikumbukwe kuwa mkamia maji hayanywi.
Mchezo huu wa leo Gatusso alimuongelea sana Ronaldo. Baadhi ya wadau wa jiji la Milan walijipiga kifua wakisema “Ronaldo hajawahi kufunga San Siro” wakasahau kuwa Waswahili husema “Mchezea matope humrukia”