Rosa Ree Ataja Sababu Za Kuonekana Kuwa Mgumu


Msanii wa muziki wa hip hop nchini anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘One way’ Rosemary Robert maarufu kama Rosa Ree amefungukia madai ya wadau wengi kuwa yeye ni mgumu.

Rosa Ree amesema kuwa watu wengi wanamuona mgumu kutokana na mavazi yake na jinsi alivyo lakini siyo kihivyo bali hapendi kujibebisha kama wafanyavyo wanawake wengine.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Rosa alisema kuna watu wengi wanamuona ana mambo ya kiume kwa sababu hajawahi kuonyesha mpenzi wake hadharani na hiyo ni sababu ya uhusiano wake wa kimapenzi kuwa binafsi zaidi.

Unajua wengi hawanielewi wanasema nina tabia za kiume lakini ukweli sipendi kujibebisha au kujilegeza na pia uhusiano wangu wa kimapenzi ni binafsi zaidi sipendi kuweka hadharani kabisa” .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad