Rose Muhando Aamrishwa Kurejea Tanzania Baada ya Video Kuibuka Mitandaoni Akiombewa Mapepo yamtoke


Taasisi inayosimamia miziki nchini Tanzania, TAMUFO imemuarisha mwanamuziki Rose muhando kurejea nyumbani mara moja baada ya video yake akiombea mapepo yamtoke ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Katibu mkuu wa taasisi hiyo Stella Joel alisema Muhando atashughulikiwa ipasavyo ikiwemo kutibiwa na madaktari kutoka India.

Akizungumza akiwa nchini Tanzania Alhamisi Novemba 22, Joel alisema Muhando ameichafulia jina taasisi hiyo kwa madai aliyoyatoa kwenye video hiyo akiombewa.


Taasisi hiyo ilidai kuwa Muhando ameichafulia jina na imeahadi kumpatia matibabu anayohitaji

" Kama taasisi,tuko na jukumu la kuangalia maslahi ya wanamuziki wote nchini Tanzania, tumeamua kuchunguza kwa kina madai aliyoyatoa mwanamuziki huyo," Joel alisema.

" Kwenye video hiyo, Muhando anasikika akimkashifu meneja wake, Nathan kwa mambo kadhaa ambayo yanaichafulia jina taasisi yetu, hivyo basi tunamtaka arejee nyumbani mara moja kwani twajua kwamba anaishi kwa mwanamuziki mmoja kutoka Kenya" Joel aliongezea.

Kulingana na katibu huyo, meneja wa Muhando ametarajiwa kufika mbele ya taasisi hiyo kujibu madai ya Muhando aliyoyatoa dhidi yake.

Aidha, taasisi hiyo ilidai kuwa inaamini Muhando hajatawaliwa na nguvu za giza ila huenda yuko na matatizo ya kiafya.

Joel alisema tayari wamewaita madatari kutoka hospitali ya Apollo nchini India ambao wanatarajiwa kumhudumia ili wabaini ni nini hasa kimekuwa kikimshumbua mwanamuziki huyo

By Swahili Kenya

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad