Rose Muhando anahangaika Kenya hana msaada tumsaidie - Ray C


Mwimbaji mkongwe wa Bongo Fleva, Ray C amelitaka Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) likiwa chini ya Waziri Harrison Mwakyembe na Juliana Shonza kumsaidia Muimbaji wa Injili Rose Muhando. 

Ray C ametumia ukurasa wake wa Instagram na kusema Rose Muhando anahitaji msaada ikiwa amepeperusha bendera ya Tanzania kupitia Muziki wake. 

"Wasanii wenzangu na watanzania kwa ujumla tunamsaidiaje dada yetu....Huyu ni wa kwetu sisi.Naamini kila mtu ana majukumu na shughuli za hapa na pale,lakini huyu dada ni mtanzania mwenzetu,ni dada yetu,ni ndugu yetu, anahangaika tu huko kenya hana msaada..Waimba injili wote,wasanii wote na watanzania kwa ujumla tunamsaidiaje dada yetu.@basata.tanzania @harrisonmwakyembe @juliana_shonza," alichapisha Ray C. 

"Naamini akipelekwa sehemu anayofaa kuwa atapata msaada,atapona na atasimama tena.Ushuhuda wangu Unatosha kuamini inawekazana1. Amepeperusha sana bendera yetu nje ya nchi kupitia muziki wake. 2.Ametupa amani ya moyo miaka na miaka kupitia muziki wake. 3.Ametusaidia sana kiimani kwa nyimbo zake. 4.Tulifarijika pindi tuskiapo nyimbo zake." 

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani Basata mpaka iambiwe na Ray ndo ichukue hatua? Mbona mambo mengine inarespond hahaha? Km Basata ni slow je mtanzania yeyote apatapo taabu ugenini ni taasisi gani inayopaswa kuingilia Kati? Je kanisa, fellowship alizokuwa akishiriki Rose ziko wapi? Juzijuzi Mbasha ulirespond haraka sana kuelezea masikitiko yako juu ya mchungaji aliyemuombea Rose. Ulisema ni jukumu lako kwa nafasi uliyonayo katika tasnia hiyo. Je Mbasha hiyo nafasi yako inaruhusu kusema tu na si kumsaidia Rose

    ReplyDelete
    Replies
    1. Je ubalozi wa Tanzania Kenya unafanyaje juu ya rose au ndo tayari inakamilisha mchakato?

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad