RUFAA ya dhamana ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko imesikilizwa leo asubuhi Alhamisi Novemba 29, 2018, katika Mahakama Kuu Dar es Salaam chini ya Jaji Sam Rumanyika, imeshindikana kutolewa uamuzi leo hadi kesho.
Akizungumza baada ya kusikiliza hoja za kisheria juu ya watuhumiwa hao kupatiwa rufaa Jaji Rumanyika amesema atazipitia hoja zote za pande mbili ili kujiridhisha hivyo atatoa uamuzi wa rufaa hiyo kesho saa nne.
Rufaa ya kesi hiyo ilifunguliwa baada ya kesi inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi ya kufanya maandamano bila kibali.
Rufaa ya Mbowe, Matiko Ngoma Ngumu Wawekewa Pingamizi
0
November 29, 2018
Tags