Sababu ya Amunike kutowapanga Mkude, Fei toto na Bocco


Baada ya kuambulia kichapo cha bao 1-0 juzi katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Lesotho, imeelezwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mnigeria, Emmanuel Amunike, aliwapanga wachezaji pekee waliokuwa wanajituma mazoezini.

Taarifa za ndani kutoka kambi ya Taifa Stars iliyokuwa huko Afrika Kusini kwa takrirani siku zinasema Amunike aliamua kuwapa nafasi wale waliokuwa wanajituma kupiga tizi la maana pekee.

Maamuzi ya Amunike kuwapanga wachezaji hao yaliwafanya wale wazoefu na waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kucheza mchezo huo kupigwa chini na Mnigeria huyo.

Kitendo cha kuwaweka benchi wachezaji kama Shiza Kichuya ambaye japo aliingia kipindi cha pili wakati Stars ikiwa imelala pamoja na John Bocco, Shiza Kichuya, Feisal Salum 'Fei Toto' na wengine kumezua gumzo kubwa kwa mashabiki.

Wachezaji hao waliokuwa wanapewa naafsi kubwa ya kuiangamiza Lesotho imeelezwa Amunike aliamua kuwaweka pembeni baada ya kutoonesha jitihada za kujifua kwenye kambi waliyoweka huko Afrika Kusini.

Stars baada ya kukumbana na kichapo hicho, sasa itawabidi washinde mchezo ujao dhidi ya Uganda huki wakiwaombea Cape Verde kuwamaliza Lesotho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad