Sakata la ushoga:Finland Haitaiiga Denmark Kuzuia misaada Tanzania


Waziri wa Mambo ya Nje nchini humo amesema hayo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kutaka kupewa majina ya wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ili wachukuliwe hatua za kisheria
-
Hata hivyo, Finland imesema haitasimamisha misaada yake ambapo kwa miaka kati ya 2016 hadi 2019 Tanzania imepangiwa kupokea Euro Milioni 52 kutoka kwa Serikali ya nchi hiyo
-
Theresa Zitting, Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika amesema "Kukiwa na hali kama hii nchini Tanzania sio hali ya kawaida kwetu sisi lakini hatuhisi kama tunahitaji kugusa maendeleo yanayofanyika kwa sasa"
-
Amesema Finland inaguswa na masuala ya haki za binadamu na lengo lake kubwa ni kusambaza na kusisita haki hizo, lakini kukatisha misaada kwa Tanzania kutaumiza Watanzania Milioni 25(Takribani 40% ya Watanzania) walio kwenye umasikini mkubwa
-
Aidha, ameongeza kwa kuwa Makonda hajapata msaada kutoka kwa Serikali hivyo wanaamini matamko yale yalikuwa ya kisiasa tu - #regrann

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad