Serikali imesema inatarajia kuanzisha mfumo maalum wa matibabu ya bima kwa Jeshi la Wananchi la Tanzania JWTZ ili kuwafanya wanajeshi kuwa na uhakika wa kupata huduma kupitia mfumo wa bima wa taifa.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Ulinzi Dkt Hussein Mwinyi akijibu swali la Mbunge wa Rashid Kuachua ambaye alihoji kuwepo kwa malalamiko ya wanajeshi juu ya kutounganishwa kwenye mpango wa bima ya afya.
Akijibu swali hilo Waziri wa Ulinzi Dkt Hussein Mwinyi amekiri kuwepo kwa malalamiko ya huduma ya tiba katika hospitali za jeshi na kuongeza hivi karibuni wataanza mfumo huo.
“Ni kweli kuwa yapo matatizo juu ya huduma za tiba kwenye hospitali za jeshi kunakosababishwa na gharama ya fedha kutokana na hayo mapungufu serikali inamalizia taratibu ili kupata ridhaa ya kuwa na bima kwa ajiili ya jeshi la ulinzi la Tanzania.” Amesema Waziri Mwinyi
Aidha Waziri Mwinyi amesema “mfuko huo wa jeshi hautaleta mgongano wa kimaslahi baina yake na mfuko wa taifa na lengo kubwa ni kuendelea kuimarisha jeshi letu.” Ameongeza