Serikali Yatangaza Mabilioni Iliyowalipa Wakulima wa Korosho

Serikali Yatangaza Mabilioni Iliyowalipa Wakulima wa Korosho
Serikali imetangaza kuongeza kasi ya malipo ya wakulima wa Korosho na kufikia kiasi cha shilingi Bilioni nne (4) kila siku ili kufanya zoezi hilo la malipo kukamilika haraka zaidi.


Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mkutano wa bodi ya korosho mkoani Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali kwenye ununuzi wa korosho za wakulima.

Amesema kuwa zoezi hilo limeenda sambamba na ongezeko la wataalamu kwaajili ya kuongeza nguvu ya malipo huku akisisitiza kuwa wataalamu wengine tayari wamekuwa na uzoefu wa namna ya kuhakiki na namna ya kulipa tangu kuanza kwa zoezi hilo.

Katika hatua nyingine, mhe Hasunga amesema kuwa serikali imejipanga kuwatambua wakulima wote wa korosho nchini ili kurahisisha kuwahudumia na kuainisha tathimini mahususi ya wakulima hao nchini.

“Jambo hili la takwimu kwenda kinyume linatupa uhakika kwamba kuna taarifa zilikuwa zinapikwa ili kumnyonya mkulima lakini changamoto zingine ambazo zimetukumba ni pamoja na uchache wa maghala kwani yaliyopo hayatoshi,” amesema Hasunga.

“Kuna changamoto za mgomo wa wapakuaji na wapakiaji wa mizigo, nasi kama serikali tutakuwa na kikao hivi karibuni na wasafirishaji ili kuhakikisha kuwa wanalipwa fedha zao haraka iwezekanavyo baada ya kupitia mikataba yao kujiridhisha jinsi walivyokubaliana”

Katika vyama hivyo vilivyohakikiwa, tayari malipo yamefanyika kwa vyama 97 ambapo wakulima 22,269 wameshalipwa huku kiasi cha korosho ambazo zimekwishalipiwa ni kilo 6,712,681 ambazo zimegharimu jumla ya Shillingi Bilioni 22.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad