Msanii wa muziki wa Bongo fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohamedi maarufu kama Shilole, ameweka wazi sababu za kutozaa na mume wake anayejulikana kwa jina la uchebe, licha ya kwamba ni muda mrefu umepita tangu wawili hao wafunge ndoa.
Akizungumza na www.eatv.tv, Shilole amesema kwamba kitendo cha yeye kutozaa na Uchebe mpaka sasa ni kwamba mipango ya Mungu haijatimia, kwani watoto hutoka kwa Mungu.
Shilole ameendelea kwa kusema kwamba wawili hao wamekuwa wakijaribu mara kwa mara kupata mtoto lalkini mpaka sasa bado, hivyo wakati muafaka ukifika ana imani ataweza kumzalia mume wake huyo.
“Sisi tulikuwa tunatafuta tupate mtoto lakini bado hatujajaliwa, unajua mtoto sio kwamba mtu anapachikwa tu, mtoto anatafutwa, na hatafutwi siku moja, watu wanakaa hata miaka 10 na hawapati mtoto na wako kwenye ndoa, mimi tayari nina watoto na hata hao wengine hawakupatikana hivi hivi”, amesema Shilole.
Msanii huyo ambaye siku za hivi karibuni ameachia kazi mpya ya 'Rap', alifunga ndoa na Uchebe kwa takban mwaka mmoja sasa, lakini hakuna dalili yoyote ya wawili hao kuwa na mtoto wao pamoja.