Shilole Atolea Povu Vyombo vya Habari Wanaowapa Umaarufu Watu Wasio na Vipaji

Shilole Atolea Povu Vyombo vya Habari Wanaowapa Umaarufu Watu Wasio na Vipaji
Msanii wa Bongofleva Shilole amelalamikia vyombo vya habari kwa kuwapa nafasi watu wasio na vipaji na kupata umaarufu na baadae kujiita wasanii ambao mwisho wa siku huharibu sanaa na kufanya vituko ambavyo vina aibisha wasanii.

Akiongea kupitia eNEWZ Shilole amesema anachukizwa sana na vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikikazana kuwapatia umaarufu watu ambao hawana sifa za kuwa wasanii na kujikuta mwisho wa siku wanaharibu kabisa sifa ya sanaa na kuharibu 'brand' za wasanii wengine waliojituma zaidi kwenye sanaa zao ili kujitengenezea umaarufu.

"Kwa kweli mimi naumia sana ninapoona kuna watu sijui ma 'video vixen' ambao wameonekana kwenye video moja halafu wanaitwa wasanii nguli ambao wakati ukiangalia hakuna kazi yoyote ya kueleweka ambayo wameifanya kwa jamii, kwa kweli mimi naomba vyombo vya habari viangalie watu wa kuwapa umaarufu ili kulinda 'brand' zetu"aliongea Shilole.

Pia Shilole amefunguka kuhusu juhudi  zake za kutaka kupungua na kubadilisha muonekano wake na kudai alishafanya mazoezi na kuacha baada ya ratiba zingine kuingilia na pia alikiri kuwa mwili wake ulivyo sasa haumpi tatizo kwani ni mwepesi na hapati shida katika kazi zake lakini anatarajia kurudi 'gym' ili kutengeneza mwili wake vizuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad