Sikukuu ya Maulid Rais Ampa Neno Lugola

Sikukuu ya Msulid Rais Ampa Neno Lugola
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amempongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola kwa kazi anayoifanya ya kuhakikisha nchi inaondokana na Uhalifu nchini.

Pongezi hizo za Dk. Shein ameitoa wakati alipokutana na ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi walipofika ikulu ya Zanzibar, alipokuwa akizungumza na viongozi hao, Dk. Shein amesema kuwa Zanzibar iko salama hali ambayo imewezesha wananchi wake waendelee kuishi kwa amani na utulivu mkubwa.

Dk. Shein amesema hatua hiyo inatokana na juhudi kubwa zinazoendelea kuchukuliwa na vikosi vyote vya idara zilizomo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi likiwemo Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Idara ya Vitambulisho vya Taifa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein, jana amejumuika na mamia ya waumini wa dini ya kiislamu kutoka Mikoa yote ya Unguja, kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

Maadhimisho hayo yalifanyika katika viwanja vya Maisara mjini hapa, ambapo Viongozi mbali mbali wa dini na Serikali, Mabalozi na wanafunzi kutoka Madrasa na Vyuo vya Quran walishiriki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad