Simba Kuwafuata Kibabe Mbabane Swallow Jumapili

Simba Kuwafuata Kibabe Mbabane Swallow Jumapili
BAADA ya kuwatembezea kichapo kitakatifu Mbabane Swallow, juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kikosi cha Simba kinatarajia kuwafuata wapinzani wao keshokutwa Jumapili kwa ajili ya mchezo wa marudiano.



Mechi hiyo ambayo inatara­jiwa kuwa na ushindani mkubwa itachezwa Desemba 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ma­vuso Sport Centre uliopo jijini Mbabane nchini Eswatini.



Hata hivyo, habari za kua­minika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Ijumaa limezipata zimedai kuwa uongozi wa timu hiyo chini ya mwekezaji mkuu wa klabu hiyo, bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ unaji­panga kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mchezo huo wa marudiano.



Imeelezwa kuwa baada ya mechi hiyo ya juzi ambayo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1, uongozi huo umetuma mtu nch­ini Swaziland kwa ajili ya kuweka mambo sawa ili timu hiyo itaka­pofika isikumbane na changa­moto yoyote kama ilivyokuwa kwa Azam FC mwaka jana.


Wakati Azam FC ilipokuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baadhi ya viongozi pamoja na wachezaji wa timu hiyo walikumbana na kichapo kutoka kwa mashabiki wa Mbabane Swallows wakati walipoenda nchini humo kwa ajili ya mchezo wa marudiano.



Hali hiyo inadaiwa kuwa moja ya chanzo cha timu hiyo kujikuta ikifungwa mabao 3-0 baada ya wachezaji kuvurugwa kisaikolojia na vurugu hizo na kujikuta wak­itupwa nje ya mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-1.



“Kwa hiyo uongozi hautaki hilo litokee na umebaini kuwa baada ya kipigo hicho ambacho wamekipata hapa nyumbani watajipanga vilivyo huko kwao kuhakikisha wa­nalipa kisasi.



“Kama ilivyo desturi yao watahakikisha wanafanya kila jambo kupitia kwa mashabiki wao ili tu waweze kututoa mchezo­ni, kwa hiyo, uongozi umejipanga kwa hilo ndiyo maana mtu huyo kaagizwa kwa ajili ya kuweka mambo sawa,” kilisema chanzo hicho cha habari.



Hata hivyo, Mratibu wa Simba, Abbas Ally alipoulizwa kuhusiana na hilo alisema: “Ni kweli kabisa tuna­jipanga vilivyo kwa ajili ya mechi hiyo ya marudiano lakini pia kukabiliana na kila hila ambayo tutakum­bana nayo tutaka­pokwenda kwao, hata hivyo mambo mengine kwa sasa siwezi kuyazungumzia.”

Stori Sweetbert Lukonge

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad