Simba yasema haiwajui Mbabane Swallows

Simba yasema haiwajui Mbabane Swallows
Klabu ya soka ya Simba imesema kuwa haiwajui vizuri wapinzani wao Mbabane Swallows lakini imejiandaa kupata ushindi kwa mazingira yoyote katika mchezo wao kwa raundi ya awali wa ligi ya mabingwa kesho.


Hayo yamesemwa na kocha wa makipa wa klabu hiyo, Mohamed Moharami ambaye amebanisha kuwa Simba imefanya maandalizi mazuri ikitambua kuwa mchezo huo wa kesho wanahitaji kushinda.

''Tunawaheshimu wapinzani wetu japo hatuwajui vizuri ila tupo tayari kwa mchezo na wachezaji wetu wako vizuri isipokuwa Shomari Kapombe na Asante Kwasi ambao ni majeruhi lakini waliobaki wote wapo vizuri kwaajili ya mchezo'', amesema Moharami.

Simba inarejea kwenye klabu bingwa baada ya misimu takribani mitano kupita ambapo msimu wa mwaka jana ilicheza kombe la shirikisho na kutolewa katika hatua za awali na klabu ya Al Masry ya Misri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad