Singida United Yanasa Sain ya Mshambuliaji was Liberia Kuongeza Nguvu

Singida United Yanasa Sain ya Mshambuliaji was Liberia Kuongeza Nguvu
Klabu ya Singida United imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji raia wa Liberia, Dauda B kwaajili ya kuongeza makali katika safu yake ya ushambuliaji.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo, Festo Sanga, mshambuliaji huyo ni moja ya mkakati wa wanaalizeti hao kujiimarisha kwa kipindi hiki kidogo ili kurejesha makali yao na hasa wanapoelekea kwenye michuano ya Sportpesa Cup mapema Januari 2019.

Singida United imeanzisha kampeni ya "Make Singida United great again" yenye lengo la kuifanya klabu hiyo kuwa na makali yake iliyokuwa nayo katika msimu wa kwanza ilipopanda ligi kuu Tanzania bara.

Klabu hiyo imekuwa na wakati mgumu katika kufunga mabao ya kutosha msimu huu, baada ya kuondokewa na wachezaji wake muhimu akiwemo Shafik Batambuze, Deus Kaseke na Tafadzwa Kutinyu. Mpaka sasa ina uwiano wa ( -1 ) magoli ya kufungwa na kufunga, ikiwa imefungwa mabao mengi zaidi kuliko ambayo imefunga.

Katika hatua nyingine, Singida United inatarajia kushusha wachezaji wengine ndani ya dirisha hili dogo ili kuimarisha nafasi mbalimbali ambazo wachezaji wake wameondoka klabuni hapo kwa kuuzwa kutokana na madai na wengine kukosa namba ya kucheza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad