Singida Yanasa Wachezaji Hawa Wanne wa Kimataifa

Singida yanasa wachezaji hawa wanne wa kimataifa
Klabu ya Singida United alfajiri ya leo siku ya Jumatano imewapokea wachezaji wapya wanne watakao ungana na timu hiyo katika harakati za kuwania ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu huu wa mwaka 2018/19.

Kupitia ukurasa wao wa kijamii wa Instagram Singida imethibitisha kuwapokea wachezaji wachezaji hao.

Wachezaji wetu wanne wakimataifa wametua nchini alfajiri hii tayari kwa kuanza kazi.Walipokuwa angani wamekutana na mchezaji wetu wa Zamani @ally_nganzi_24 (kushoto) anayekipiga Jamhuri ya Czech ambaye amerejea nchini kwa mapumziko ya wiki tatu.

Singida imewapokea wachezaji hao wanne wa kimataifa wa Zambia walio tuwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa  wa JK na sasa tayari kukamilisha taratibu zilizo baki wachezaji hao ni mabeki wawili wa pembeni, Mshambuliaji moja na kiungo mkabaji mmja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad