"Sipendi Uchokozi" Kauli ya Trump kwa Urusi

"Sipendi Uchokozi" Kauli ya Trump kwa Urusi
Rais wa Marekani Donald Trump amesema huenda akafutilia mbali mkutano baina yake na rais wa Urusi Vladimir Putin kufuatia mzozo kati ya taifa hilo na Ukraine.

Trump ameliambia gazeti la Washington Post kuwa anasubiri "ripoti kamili" baada ya Urusi kuvurumiza moja ya meli ya Ukraine na kuteka zingine tatu siku ya Jumapili.

Ukraine inasema hiyo ni ''hatua ya uchokozi', huku Urusi nayo ikisema meli hizo ziliingia kiharamu katika mipaka yake majini.

Mhadhiri aliyetaka kufikisha ujumbe kwa Magufuli UDSM
Magufuli awasifu Wachina, misaada yao 'haina masharti'
Msisimko wa kilimo cha bangi Lesotho
Sheria ya kijeshi imewekwa katika baadhi ya sehemu ya Ukraine.

Huku hayo yakijiri Marekani imetoa wito kwa mataifa ya Ulaya kuisaidia Ukraine.

Mzozo wa sasa umezuka vipi?
Siku ya Jumapili meli za kivita za Berdyansk na Nikopol, pamoja na meli ya kuzisindikiza Yana Kapa, zilijaribu kusafiri mji wa bandarini kwenye Bahari Nyeusi wa Odessa kuelekea Mariupol katika Bahari ya Azov.

Ukraine inasema Urusi ilijaribu kuzizuia meli hizo zisiendelee na safari yake, ambapo meli moja iliigonga meli ya Yana Kapa.

Meli hizo ziliendelea na safari kuelekea mlango wa bahari wa Kerch, lakini zikapata njia imezibwa na meli moja kubwa.

Urusi wakati huo ilikuwa imetuma ndege mbili za kivita na helikopta mbili ambazo zilikuwa zikipaa angani katika eneo hilo na kufuatilia mwenendo wa meli hizo.

Haki miliki ya pichaAFP
Image caption
Volodymyr Lisovyi ni mmoja wa wanaume watatu waliyotoa taarifa kwa lazima kwa mkuu wa jeshi la maji la Ukraine
Urusi inaituhumu Ukraine kwa kuingia kinyume cha sheria katika maeneo yake ya bahari na usafiri eneo hilo umesitishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu za kiusalama.

Jeshi la wanamaji la Ukrane lilisema meli hizo zilikuwa zimeshambuliwa na kuharibiwa zilipokuwa zinajaribu kuondoka eneo hilo.


Siku ya Jumanne, Rais Petro Poroshenko alisema kuna tishio la ''vita kamili" kati yetu na Urusi.

"Idadi ya magari ya kivita ya Urusi yameongezeka katika mara tatu zaidi katika kambi yake ya mpakani," alisema.

Usiku ya Jumatatu, bunge la Ukraine liliunga mkono auamuzi wa rais Poroshenko wa kuweka sheria ya kijeshi kwa siku 30 katika maeneo 10 ya mpakani kuanzia Novemba 28.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad