Spika Ndugai Amtupia Dongo Mchungaji Msigwa "Namuona Mh. Msigwa Inamuuma Sana''

Spika Ndugai Amtupia Dongo Mchungaji Msigwa "Namuona Mh. Msigwa Inamuuma Sana''
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amempa dongo mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa kwa kumwambia anaumia kumuona mbunge mpya wa CCM Joseph Mkundi wa Ukerewe akichangia bungeni.

Ndugai ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma kwenye kipindi cha maswali na majibu ambapo alimkaribisha kuuliza swali mbunge huyo aliyeapishwa leo Novemba 15, 2018.

“Karibu Mheshimiwa mbunge mpya kabisa wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jimbo la Ukerewe Joseph Mkundi, namuona mheshimiwa Msigwa inamuuma sana'', alisema Spika Ndugai.

Mbunge huyo wa Ukerewe Joseph Mkundi ameapishwa leo Bungeni, baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo wa Ubunge uliofanyika hivi karibuni kufuatia mbunge huyo kujiuzulu nafasi yake akiwa CHADEMA na kuhamia CCM kisha kugombea tena.

Katika swali lake alihoji ni lini serikali itapeleka gari la wagonjwa katika kituo cha afya cha Bwisya, ambacho kilitumika kuhudumia wahanga wa ajali ya MV Nyerere mapema mwezi Agosti.

Swali hilo lilitolewa majibu na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ambaye alisema serikali itanunua magari ya wagonjwa 70 na moja litapelekwa katika kituo hicho cha Afya kama ilivyoelekezwa na Rais Magufuli.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad