Sugu Atangaza Kufuata Nyayo za Kikwete

Sugu Atangaza Kufuata Nyayo za Kikwete
Mbunge Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesema anakaribia kukamilisha kitabu chake alichokipa jina la Siasa kutoka bungeni hadi kufungwa jela (siasa from the Parliament to prison) na kueleza kitabu hicho kitaelezea maisha yake akiwa gerezani.

Kwa mujibu wa Sugu kitabu hicho pia kitachambua masuala mengine mbalimbali, ikiwemo uendeshaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha Spika, Job Ndugai, na namna ambavyo amekuwa akishirikiana na viongozi wa kiserikali.

“Kitabu changu cha sasa kitaelezea uzoefu wangu kwenye uendeshaji wa Bunge, na yanayoendelea bungeni kwa sasa, na mpaka nilipokamatwa na kupewa kesi ya kufungwa kisiasa, nitaandika maisha yangu ya gerezani kama mfugwa, nitaandika matukio makubwa yaliyonitokea nikiwa gerezani.”

Hivi karibuni kupitia www.eatv.tv Sugu alisema kuwa anatafuta picha yake akiwa gerezani na kutangaza kutoa donge nono la milioni tano kwa atakayempatia picha yake akiwa gerezani.

“Timu yangu  inahangaika na ndiyo  maana tumetangaza kuanzia milioni  3 hadi milioni 5, kwahiyo nasisitiza atakayeipata atuletee, mara moja ili nikamilishe kitabu changu,” aliongeza Sugu.

Sugu ni miongoni mwa wanasiasa wachache, nchini ambao wamekuwa na utaratibu wakuandika vitabu vyenye historia yao akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete ambaye amekuja na kitabu chake kitakachoitwa kutoka mwanafunzi mtembea peku hadi urais.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad