Tanzania Yadaiwa Kumtimua Balozi wa Umoja wa Ulaya

Tanzania Yadaiwa Kumtimua Balozi wa Umoja wa Ulaya
BALOZI wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland Van de Geer raia wa Uholanzi, anadaiwa kupewa hadi leo Novemba 3, 2018 awe ameondoka kwenye Ardhi ya Tanzania huku sababu rasmi za kuondolewa kwa balozi huyo bado hazijawekwa wazi.



Aidha, inaelezwa kuwa msaidizi wa balozi huyo, Charles Andrew-Stuart anachukua mikoba kwa muda wakati hatua zaidi zikichukuliwa.



Wakati huohuo, bila ya kukanusha wala kuzikubali taarifa za awali zinazodai kafukuzwa nchini, EU imesema Balozi Roeland van de Geer atasafiri kwenda Brussels nchini Ubelgiji kujadili hali ya kisiasa nchini Tanzania wiki ijayo.



Ubalozi pia umesema Roeland anaenda kukutana na maofisa wa ngazi za juu wa umoja huo kujadili pia ushirikiano wa baadaye kati ya EU, wanachama wake na Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad