Tanzania Yadaiwa Zaidi ya Tsh Bilion 400 Kwenye Mahakama za Kimataifa


Serikali ya Tanzania inakabiliwa na kesi za madai ya jumla ya Dola za Marekani 185,580,009.76 kutoka na mashauri 13 yaliyofunguliwa kwenye Mahakama za kimataifa

Hata hivyo, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema licha ya gharama hiyo hakuna shauri lililotolewa uamuzi hivyo fedha hizo si madeni halisi

Waziri Kabudi alitoa kauli hiyo bungeni jana Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe aliyetaka kujua pia Serikali imejifunza nini kutokana na kesi hizo

Waziri Kabudi alisema mashauri hayo yalifunguliwa kuanzia Novemba 2015 katika Mahakama mbalimbali zikiwamo Permanent Court of Arbitration(PCA), London Court of International Arbitration (LCIA) na International Centre for Settlement of Investment Dispute (ICSID)

Aidha, aliongeza kuwa hakuna kesi iliyofunguliwa na kampuni ya Acacia Mining na kwamba shauri namba UN 173686 na Shauri UN 1736867, yamefunguliwa Julai 3 na kampuni ya Pangea Minerals Ltd na Bulyanhulu Gold Mining Ltd
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad