Timu ya taifa ya soka la Ufukweni ya Tanzania imefanikiwa kushinda ubingwa wa Copa Dar es salaam kwa kuifunga timu ya taifa ya Uganda katika mchezo wa fainali.
Mashindano hayo yaliyofanyika katika fukwe za Coco jijini Dar es salaam yamemalizika jioni ya leo, Novemba 25 kwa Tanzania kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 didi ya Uganda na kushida ubingwa huo wa kwa mara ya kwanza tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka uliopita.
Nafasi ya tatu imekwenda kwa timu ya taifa ya Seychelles baada ya kuifunga timu ya taifa ya Malawi kwa penati 4-3 kufuatia sare ya mabao 8-8 katika muda wa kawaida.
Mwaka uliopita ambapo mashindano hayo yalifanyika kwa mara ya kwanza ilishuhudiwa Zanzibar ikishinda ubingwa kwa kuichapa Malawi kwa mabao 3-2. Mashindano ya mwaka huu yalishirikisha nchi za Tanzania, Malawi, Seychelles na Uganda.