Shirikisho la Mpira wa miguu nchini ‘TFF’ imeiandikia barua klabu ya Yanga kubadili jina lake kutoka ‘Sports Club’ na kuitwa ‘Football Club’.
Yanga maarufu kama Young Africans Sports Club imetakiwa kutoa maneno hayo ya mwisho ambayo tafsiri yake hujumuisha michezo yote wakati kikanuni kutoka Shirikisho la soka duniani ‘FIFA’ ni makosa.
TFF ikitoa ufafanuzi swala hilo, FIFA inajihusisha na mchezo wa soka pekee kwa wanaume na wanawake na si michezo mingine hivyo kutumia jina ‘ Sports Club ‘ lenye maana ya ya klabu inayojihusisha na michezo mbalimbali ikiwemo soka ni makosa.
Kama hayo yatatekelezwa klabu ya Yanga itatambulika kama Young Africans Football Club, katika habari hiyo iliyoenea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii itaihusu pia Simba ambao hutumia jina la Simba Sports Club.