Tshishimbi aitesa Yanga kwa Hili

Tshishimbi aitesa Yanga kwa Hili
WAKATI kikosi cha Yanga jana kikianza tena mazoezi baada ya mapumziko ya siku moja, kiungo Papy Kabamba Tshishimbi, bado anaendelea kuuguza majeraha yake ya goti na uongozi wa timu hiyo haujui atarejea lini uwanjani, imeelezwa.

Wiki hii Yanga ilishuhudia majeruhi mwingine, Ibrahim Ajibu, Andrew Vincent na Juma Abdul wakirejea uwanjani, lakini hali bado imekuwa ngumu kwa Tshishimbi na Juma Mahadhi.

Akizungumza na Nipashe jana muda mfupi baada ya kumalizika mazoezi ya asubuhi ya kikosi hicho, Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema maumivu ya goti bado yanamsumbua Tshishimbi ambaye yupo nje ya uwanja akiendelea na matibabu.

"Tshishimbi bado kwa kweli..., goti bado linamsumbua na anaendelea na matibabu, sifahamu lini anaweza kurejea uwanjani," alisema Saleh.

Alisema ukimwondoa Tshishimbi na Mahadhi, wengine wanaendelea na mazoezi huku pia wakikosekana nyota wa timu hiyo walioitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa.

"Tumeanza tena mazoezi leo na kocha Zahera, lakini yeye muda wowote anaondoka kwenda kwenye majukumu ya timu yao ya taifa," alisema Saleh.

Kwa upande wake, Zahera, alisema angependa kuona wachezaji wake wote wanakuwa kwenye hali nzuri ili kumpa wigo mpana wa kupanga kikosi chake.

"Nimefurahi Andrew Vincent, Ajibu na Juma wamerejea na mchezo uliopita wamecheza..., natamani pia kuona Tshishimbi na wengine wanapona na kurejea uwanjani, hii itasaidia kupanga kikosi chetu vema kulingana na mchezo," alisema Zahera.

Aidha, alisema wakati wowote ataenda kuungana na timu ya Taifa ya DR Congo inayojiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Afrika utakaochezwa Novemba 18 Brazzaville.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad