Urusi imezishambulia na kuziteka meli tatu za kivita za Ukraine zilizokuwa baharini katika rasi ya Crimea katika kisa ambacho kimezidisha uhasama baina ya mataifa hayo mawili.
Meli mbili ndogo za kivita, pamoja na meli moja ya kusindikiza meli ndizo zilizotekwa na wanajeshi wa Urusi.
Vifaru vya Urusi vinavyoitia wasiwasi Nato
Mazoezi ya kijeshi ya Urusi na Belarus yaanza
Putin asema Urusi ina kombora lisiloweza kuzuiwa
Leo Jumatatu, wabunge wa Ukraine wanatarajiwa kupiga kura kuidhinisha kuanza kutekelezwa kwa sheria za kijeshi.
Mzozo wa sasa ulianza pale Urusi ilipoituhumu Ukraine kwa kuingiza meli katika maeneo yake ya bahari kinyume cha sheria.
Urusi kisha iliweka meli kubwa ya kusafirisha mizigo na kuziba daraja la kuingia kwenye mlango wa bahari wa Kerch, njia pekee ya kuingia kwenye Bahari ya Azov na ambayo hutumiwa na mataifa yote mawili
Wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama na Ulinzi la Ukraine, Rais Petro Poroshenko alieleza vitendo vya Urusi kuwa "uchokozi usio na sababu na za kiwendawazimu."
Urusi imeomba kuandaliwe mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mkutano ambao balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema umepangiwa kufanyika saa tano asubuhi saa za New York (16:00 GMT) leo Jumatatu.
Urusi Yateka Meli za Kivita za Ukraine, Rais Petro Poroshenko Ataka Sheria za Kijeshi, UN kukutana
0
November 26, 2018
Tags