Vikao vya Bunge Vyaanza Leo Dodoma Waitala, Kalanga na Mzava Waapishwa

Vikao vya Bunge Vyaanza Leo Dodoma Waitala, Kalanga na Mzava Waapishwa
Mkutano wa 13 wa Bunge umeanza leo Jumanne, Novemba 6, 2018, huku wabunge wanne wawakiapishwa na Spika Job Ndugai, ambao wote ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Thimotheo Mzava (Korogwe Vijijini), Mwita Waitara (Ukonga), Julias Kalanga (Monduli) na Zuberi Kuchauka (Liwale).


Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema miswada ya sheria mitano itasomwa kwa mara ya kwanza ikiwemo wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2018, mswada mingine ni wa maji na usafi wa mazingira, marekebisho ya sheria mbalimbali namba nne wa mwaka 2018, muswada wa mamlaka ya hali ya hewa wa mwaka 2018 na wa mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu.

Pia kuna muswada wa sheria za huduma ndogo za fedha wa mwaka 2018 ambao utasomwa katika hatua zake zote. Hati ya dharura ya mheshimiwa Rais ambao kamati ya uongozi imeridhia kusomwa katika hatua zake zote.

Aidha, katika mkutano huo mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa mwaka 2019/20 utajadiliwa na sehemu kubwa mijadala itajikita katika mpango huo. Pia, maswali 125 yataulizwa na ya papo kwa waziri mkuu yatakuwa 16.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad