Wachezaji was Yanga Wamtumia Salamu za Pole Kapombe

Wachezaji was Yanga Wamtumia Salamu za Pole Kapombe
Baada ya beki wa kulia wa Sim­ba, Shomari Kapombe, kufanyiwa upasuaji wa mguu kufuatia kuu­mia enka kwenye kambi yaT­aifa Stars nchini Afrika Kusini wachezaji na mashabiki wa Yanga wamemuombea dua apone haraka.

Kapombe alilazimika kubakia nchini humo kwa ajili ya kupatiwa matibabu, na tayari alifanyi­wa upasuaji wa mguu wake katika hospitali moja kubwa kwenye Jiji la Pretoria, Afrika Kusini.


Mrisho Ngassa kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa ana imani beki huyo atarejea katika hali yake na Mungu atamsaidia apone.

Juma Abdul nahodha msaidizi wa Yanga naye pia alisema kuwa ni mapito ambayo wachezaji wanapitia hivyo Mungu atamsaidia atakuwa salama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad