Wachina Watatu Wanaofanya Kazi Shirika la Relief Kenya Mbaroni kwa Rushwa

Raia watatu wa China wanaofanya kazi na Shirika la Reli nchini Kenya watafikishwa mahakamani baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika kwenye sakata ya tikiti katika reli ya kisasa ya SGR.

Kwa mujibu wa BBC, Li Gen, anayesimamia usafiri , Li Xiaou meneja wa ulinzi na Sun Xin, mfanyakazi wa Kampuni ya China Road and Bridge Cooperation (CRBC) waliyokamatwa Ijumaa watafunguliwa mashtaka ya kujaribu kuwahonga maafisa waliokuwa wanachunguza sakata hiyo ya tikiti.



Hii ni baada ya mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya kuidhinisha tume ya kupambana na ufisadi kuwafungulia mashtaka raia hao watatu wa China.

Watatu hao wanaripotiwa kujaribu kuwahonga maafisa wa uchunguzi shilingi 500,000 za Kenya au dola 5,000. Walikamatwa Ijumaa na maaafisa kutoka tume ya kupambana na ufisadi EACC.


Polisi wanasema wafanyabiashara wengine wamechukua wajibu wa kuwaletea wasafiri tikiti ambao hawataki kusumbuka kwa kupanga foleni ndefu.

Ukizungumzia suala hilo ubalozi wa China mjini Nairobi kupitia mkurugenzi wake wa mawasiliano Zhang Gang alisema Ubalozi unaheshimu uchunguzi unaofanywa na mamlaka za Kenya kuambatana na sheria za Kenya

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad