Wamegoma kuuza bidhaa kwa madai ya kuonewa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko kwa kuwatoza faini za mara kwa mara za Tsh. 50,000
Pamoja na faini hizo pia wamelalamika kupewa risiti zilizoandikwa mwaka 2010 na kudai kuwa ni feki na huenda pesa zao zinaliwa bure
Mgomo huo uliodumu kwa takribani saa 3, umetokea leo asubuhi baada ya DC kupita sokoni na kumtaka Afisa Afya wa Manisapaa kuwapiga faini Wafanyabiashara walioweka bidhaa chini kwa kuwa ni kinyume na sheria
Afisa Afya, Kuchibamba Kizito alikiri kupewa maagizo na DC na kutolea ufafanuzi suala la risiti kuandikwa mwaka 2010 kuwa ni kujisahau kuweka 'setting' ya mashine
Aidha, DC Jasinta Mboneko alitoweka eneo la tukio na alipopigiwa simu alisema suala hilo kwa sasa hawezi kulizungumzia bali kesho ndiyo atafanya kikao na viongozi wote wa masoko