Waitara Aanza kwa Mkwara Mzito Bungeni

Waitara Aanza kwa Mkwara Mzito Bungeni
Mbunge wa Jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Mwita Waitara ameuliza swali kwa mara ya kwanza tangu aapishwe kuwa mbunge kwa mara ya pili kupitia chama hicho tawala ikiwa miezi michache baada ya kujiuzulu nafasi hiyo akiwa ndani ya CHADEMA.

Waitara pamoja na wabunge wenzake watatu wameapishwa leo Jijini Dodoma tangu walipochagulia kupitia chaguzi ndogo ambazo zilikuwa na ushindani sana hasa katika majimbo ya Monduli, na Liwale.

Akiuliza swali kwa mara ya kwanza, Waitara amesema “ni lini serikali katika maeneo muhimu kwa wananchi wa ukonga ambao waliiheshimu CCM, wanapata umeme haraka iwezekanavyo?”

Akijibu Swali Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu amesema “serikali imeanza kazi ya kupeleka maeneo ambayo ameyalalamikia na wanatarajiwa kuwasha umeme baada ya vikao vyabunge kuisha.”

Mwita Waitara ni miongoni mwa waliokuwa wabunge wa upinzani waliokuwa na msimamo mkali lakini baadaye alitangaza kuondoka kwenye chama chake cha zamani kwa madai kutoelewana na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe lakini kwa upande viongozi wa upinzani wamesema mbunge huyo alinunuliwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad