Wakati Wabunge wapya wa CCM wakiapishwa, Wabunge wa CHADEMA, CUF wasusa


Wabunge wa Chadema na wa CUF upande wa katibu mkuu Maalim Seif wamesusia kushuhudia kiapo cha wabunge wanne wa CCM wakati wabunge hao walipokuwa wanaapishwa. 

Mkutano wa Bunge umeanziia leo asubuhi Jumanne Novemba 6, 2018 na kuongozwa na Spika Job Ndugai. 

Mara baada ya kumaliza dua na wimbo wa Taifa, uliwadia wasaa wa kiapo kwa wabunge wanne waliokuwa upinzani ambao walijiuzulu na kuhamia CCM ambako waliibuka washindi. 

Wakati wa shughuli hiyo ya kiapo, wabunge hao wa Chadema na CUF upande wa Maalim Seif hawakuwapo bungeni. 

Aliyekuwa wa kwanza kuapishwa ni Julius Kalanga (Monduli), akafuatia Mwita Waitara (Ukonga), akaja Timotheo Mzava (Korogwe vijijini) aliyepita bila kupingwa akichukua nafasi ya marehemu Stephen Ngonyani ‘Majimarefu’ aliyefariki dunia. 

Wa mwisho kuapishwa alikuwa Zuberi Kuchauka (Liwale) ambaye awali alikuwa mbunge kupitia CUF. Mara baada ya kumaliza kuapishwa, wabunge hao wa Chadema na CUF walirejea bungeni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad