Mwanasheria maarufu nchini Tanzania, Alberto Msando amefunguka muda mchache mara baada ya kamati ya maandalizi ya Tigo Fiesta mwaka 2018 kutangaza kusitisha tamasaha hilo lililopaswa kufanyika leo Novemba 24, mwaka 2018 katika viwanja vywa Leaders Kinondoni Dar es salaam.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram wakili huyo msomi ameandika kuwa maamuzi ya kutoa kibali wakati mtu anajua kuna wagonjwa wa moyo ni ya kipuuzi huku akiongeza kuwa maamuzi ya kufuta kibali cha Tigo Fiesta siku moja kabla ya tukio ni ya hovyo.
”Hatuwezi na hatupaswi kuwa nchi au mkoa ambao mfanyabiashara au mwananchi hana uhakika au hajui maamuzi gani yatatolewa kuhusu maisha yake au jambo lake lolote. Maamuzi ya kutoa kibali wakati mtu anajua kuna wagonjwa wa moyo ni ya KIPUUZI,” ameandika wakili Alberto Msando.
Wakili huoyo msomi, Msando ameongeza ”Maamuzi ya kufuta kibali cha Tigo Fiesta siku moja kabla ya tukio ni ya HOVYO. We must be consistent. Huwezi kusema na ukaeleweka kwamba ‘baada ya malalamiko ya wagonjwa’ ndio umegundua Leaders hapafai kwa tamasha! Uongozi wenye kuacha alama una sifa zifuatazo 1. USAWA 2. UKWELI 3. HAKI 4. BUSARA 5. USHIRIKISHAJI. All said, kila mmoja atajifunza. Jambo ambalo liko wazi sana ni kwamba kila mmoja wetu anayo NAFSI. HUWEZI KUIDANGANYA NAFSI YAKO.”
Mapema asubuhi ya leo uongozi wa Clouds Media kupitia kamati ya maandalizi ya Tigo Fiesta mwaka 2018 imetangaza kusitisha tukio la kilele cha msimu wa Tigo Fiesta 2018 lililopaswa kufanyika leo Novemba 24, mwaka 2018 katika viwanja vywa Leaders Kinondoni Dar es salaam.
View this post on Instagram
Hatuwezi na hatupaswi kuwa nchi au mkoa ambao mfanyabiashara au mwananchi hana uhakika au hajui maamuzi gani yatatolewa kuhusu maisha yake au jambo lake lolote. Maamuzi ya kutoa kibali wakati mtu anajua kuna wagonjwa wa moyo ni ya KIPUUZI. Maamuzi ya kufuta kibali cha Tigo Fiesta siku moja kabla ya tukio ni ya HOVYO. We must be consistent. Huwezi kusema na ukaeleweka kwamba ‘baada ya malalamiko ya wagonjwa’ ndio umegundua Leaders hapafai kwa tamasha! Uongozi wenye kuacha alama una sifa zifuatazo 1. USAWA 2. UKWELI 3. HAKI 4. BUSARA 5. USHIRIKISHAJI. All said, kila mmoja atajifunza. Jambo ambalo liko wazi sana ni kwamba kila mmoja wetu anayo NAFSI. HUWEZI KUIDANGANYA NAFSI YAKO. #TheDon.
A post shared by Msando Alberto (@albertomsando
Wakili Msomi Albeto Msandk Atoa Povu Zito Baada ya Tamasha la Tigo Fiesta Kusitishwa "Maamuzi ya Kufuta Ghafla ni Hovyo"
0
November 24, 2018
Tags