Wakulima wa Zao la Korosho Waandamana Kupinga Serikali Kununua kwa 3300

WWakulima wa Zao la Korosho Waandamana Kupinga Serikali Kununua kwa 3300
Wakulima wa zao la korosho katika wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wamelazimika kufanya maandamano maalum kwa lengo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.


Maandamano hayo ya wakulima wa korosho yametokana na hatua ya serikali kuamua kununua zao hilo kwa bei ya shilingi 3300 kufuatia kuzuka kwa mgogoro wa kibiashara baina ya wakulima na wafanyabiashara juu ya bei.

Kwa mujibu wa madai ya wakulima hao, uamuzi uliofanywa na serikali unaonesha kujali na kuthamini maslahi yao kwa kile walichokieleza kuwa utapelekea kuongeza kipato mara dufu zaidi ya kile walichokuwa wakikipata.

“Tunampigia magoti kumuheshimu Mheshimiwa Rais kwa hatua aliyoifanya ametusaidia sana naomba utusaidie kutufikishia ombi letu hilo  kwa Rais Magufuli, wewe Mkuu wetu wa Mkoa,” amesema Issa Yassin, mmoja ya wakulima waliokuwa waendamana.

Akizungumza akiwa na wakulima hao ambao waliandamana , Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera amewataka wakulima kuhifadhi kiasi cha fedha ambacho wanakiingiza kwa sasa ili kiweze kuwanufaisha kuelekea msimu ujao wa korosho.

“Kwa namna moja au nyingine niwaombe hizo pesa mnazopata mnunue pembejeo kwa ajili msimu ujao wa  korosho ili muziweke ndani,” amesema Juma Homera
 ya wanawake katika maendeleo.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad