Wakulima wafunguka kuhusu bei ya JPM ya korosho

Wakulima wafunguka kuhusu bei ya JPM ya korosho
Wakulima wa zao la Korosho Mkoani Mtwara wamefurahishwa na maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta John Magufuli, kuwa serikali inabeba jukumu la kununua zao hilo kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo.

Wakizungumza www.eatv.tv Ibrahim Sabuli na Abdurlahman Ally ambao ni wakulima korosho baada ya kusikia kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa mapema leo katika zoezi la kuwaapisha Mawaziri na Naibu mawaziri, wakulima hao wamesema awali walikatishwa tamaa na mwenendo wa hali ya ununuz wa zao hilo.

“Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kwa maamuzi aliyotufanyia wakulima wa korosho, tunamshukuru sana,” amesema Ibrahim Sabuli, ambaye ni mmoja ya wakulima hao.

Kwa upande wao, viongozi wa vyama vya msingi, Ally Mnyachi ambaye ni mjumbe wa bodi muungano AMCOS amesema kuwa,

“Hatua hiyo itaongeza kasi ya wakulima kuwasilisha korosho katika maghala yao, tofauti na ilivyokua kabla ya tamko la Rais Magufuli.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad