Idadi ya Watu waliofariki kutokana na ajali ya moto unaochoma msitu nchini Marekani imefikia 71 huku zaidi ya watu 1,011 hawajulikani walipo, Askari Kory Honea amesema hayo jana Novemba 16
Zimamoto wamejikuta wakipambana na aina mbili za moto katika msitu huo ambapo awali walikuwa walipambana na moto uliopewa jina la Camp Fire'l uliopo katika Kaunti ya Butt lakini sasa umeibuka mwingine katika Kaunti ya Ventura uliopewa jina la Woolsey Fire
Wameeleza kuwa Mvua ingezaidia kuuzima moto huo lakini ingeleta ugumu katika kuwatafuta waliopotea na kupoteza maisha kutokana na kwamba wamekuwa wakikutana na mifupa tu au vipande vya mifupa ya watu
CampFire umeharibu nyumba 9,700 na majengo 144 na hadi kufikia jana ulikuwa umezimwa kwa asilimia 45 na sehemu iliyobaki haihatarishi maeneo yenye watu wengi
Aidha, Kusini mwa California watu zaidi wamekuwa wakiruhusiwa kurudi majumbani kwao baada ya asilimia 69 ya WoolseyFire kuzimwa hadi kufikia jana usiku, moto huo umeteketeza nyumba 600