Wamarekani Wapiga Kura za Maoni Uchaguzi wa Katikati ya Muhula

Wamarekani Wapiga Kura za Maoni Uchaguzi wa Katikati ya Muhula
Wamarekani wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa kitaifa wa katikati ya muhula ambao unaonekana kama kura ya maoni kuhusu urais wa Donald Trump.

Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa kwenye Pwani ya Mashariki huku vyama vya Republican na Demoratic vikipania kuchukua udhibiti wa mabunge ya uwakilishi na Seneti.

Uchaguzi huu wa katikati ya muhula unakuja wakati rais Trump amefikia nusu ya muda wa uongozi wake madarakani.
Uchaguzi huo pia unatarajiwa kubaini ikiwa Trump ana uwezo wa kuongoza Marekani katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Shauku ya upigaji kura inatarajiwa kuchochea watu wengi zaidi kushiriki zoezo hilo.

Viti 435 katika bunge la waakilishi na viti 35 kati ya 100 katika Seneti vinakabiliwa na ushindani mkubwa.

Ijue sababu ya balozi wa EU Tanzania kuitwa nyumbani
Siku za hivi karibuni rais Trump amekuwa akitumia mbinu tofauti kuwasilisha hoja ambazo zinaonekana kuzua hisia mseto katika juhudi ya kuimarisha uungwaji mkono wake.

Aliyekuwa mtangulizi wake, Barack Obama - amekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeini za chama cha Democratic - amesema "hulka ya taifaletu iko katika sanduku la upigaji kura".


Wakati wa kampeini zake za mwisho katika majimbo ya Ohio, Indiana na Missouri, bwana Trump alirejelea masuala muhimu yaliyomsaidia kushinda uchaguzi wa mwaka 2016 akisisitiza kuwa Democrats watasambaratisha uchumi na kwa kuruhusu uhuamiaji haramu.

Wagombea wa Democratic kwa upande wao wameamua kujiepusha na makabiliano ya moja kwa moja na wapinzani wao na badala yake kuangazia masuala ibuka kama vile ya afya na ukosefu wa usawa katika mambo ya uchumi.

Chama hicho kunatumai kuwa wapiga kura vijana na wale wanaotokea katika makundi ya wachache waliyotengwa watavutiwa na kura hiyo kama hatua ya kupinga msimamo wa rais Trump dhidi ya masuala yanayo wagusa wao na wenzao moja kwa moja.

Trump amekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutokana na lugha yake ambayo inadaiwa kuwagawanya watu.

Upigaji kura wa mapema ulianza Novemba 4 katika majimbo ya Los Angeles na California
Watafiti wa kura ya maoni wanabashiri kuwa Democrats huenda wakashinda viti 23 wanazohitaji kuongoza bunge la waalikilishi , na viti vingine zaidi kama 15 za ziada.

Hata hivyo Democrats wanatarajiwa kupoteza viti viwili kupoteza nafasi hiyo ambayo itawawezesha kuchukua udhibiti wa bunge la Seneti.


Baada ya miezi kadhaa ya kampeni, uvumi na mabilioni ya dola zilizotumika kwenye matangazo, wapiga kura hatimae watakuwa na nafasi ya kufanya maamuzi yao ya mwisho siku ya Jumanne.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad