Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akamatwa na mirungi


Jeshi la Polisi mkoani Manyara, linamshikilia Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Monduli mkoani Arusha kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 20.

Akithibitisha kukamatwa kwa askari huyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Augustino Senga amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana saa 16:50 jioni maeneo ya Minjingu Kata ya Nkaiti, Wilaya ya Babati wakati askari wakiwa katika upekuzi wa magari na ufuatiliaji wa taarifa fiche.

“Wakati wanaisimamisha gari lenye namba T543DHJ, aina ya Alteza ikitokea Makuyuni, Arusha katika kizuizi cha mabasi Minjingu, ghafla gari hilo lilibadilisha mwelekeo kurudi nyuma kuelekea Arusha na ndipo askari hao walipotilia shaka na kuanza kuifukuza kwa nyuma na kufanikiwa kuikamata maeneo ya Nanja Wilaya ya Monduli ikiwa inaendeshwa na dereva mwanajeshi mwenye namba  MT. 12014 Abdul Bashiri Ally miaka 25 Askari wa JWTZ Monduli Arusha,”amesema Kamanda Senga.

Kamanda Senga amesema baada ya kuipekua gari hiyo ilikutwa ba bunda 60 za mirungi sawa na kilo 20 ikiwa imehifadhiwa kwenye buti la gari hilo.

“Mtuhumiwa amekamtwa kwa mahojiano kubaini mahali alikoitoa na kubaini mtandao wake kwani wakati anakamatwa mwenzake alishuka kwenye gari na kutoroka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad