Maafisa misitu nchini India wanajaribu kuwashika watoto wa chui milia aliyeuawa kwa hofu kuwa huenda wakageuka na kuwa wala watu.
Inaaminiwa kuwa mama yao ambaye aliuawa katika jimbo la Maharashtra baada ya msako mkubwa mwezi huu, alikuwa amewaua watu 13.
Chui milia huyo wa umri wa miaka sita alikuwa amekwepa kushikwa kwa miaka miwili.
Kuuliwa kwake kuliwaghaddhabisha watunza wanyama na kuna matumaini kuwa watoto wake wawili wa umri wa miezi 11 wanaweza kudungwa dawa ya kulala ili washikwe.
"Wanaweza kuokolewa kwa sababu wanaweza kugeuka kuwa wala watu," mkuu wa utunzaji misitu AK Misra jimbo la Maharashtra alisema.
Kuwindwa kwa chui milia huyo kwa jina T-1 kulihusu zaidi ya kamera 100, farasi na mbuzi waliofungwa kwenye miti kama mtego kila wakati na doria za maafisa waliojihami.
Maafiss wa wanyama pori kisha wakaleta marashi ya Calvin Klein, ambayo uchunguzi nchini Marekani ulionyesha kuwa yangeweza kuwavutia chui.
Mwezi Agosti chui milia huyo aliwaua watu watatu kwenyr mji wa Pandharkawada wilaya ya Yavatmal na kuwaacha zaidi ya wenyeji 5000 wakishi kwa hofu.
Wenyeji walikuwa na wasi wasi kuwa watoto hao wa chui milia walikuwa wameonja damu ya watu.
Mara watakapokamatwa mamlaka zitaamua ni wapi watapelekwa.
India ni nyumbani kwa asilimia 60 ya chui milia wote walio duniani. Kuna zaidi ya chui milioa 200 katika jimbo la Maharashtra.
Watunzaji wanasema sehemu zao za kuishi zinapungua kwa sababu ya shughuli za mwanadamu.