Watu 14 Kizimbani kwa Tuhuma Ulanguzi wa Korosho


WATU 14 wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tunduru, kwa tuhuma za kukutwa wakifanya biashara ya ununuzi wa korosho kupitia mfumo usio rasmi, maarufu kama Kangomba.

Sambamba na watuhumiwa hao, pia yumo Mohamed Wadali, anayekabiliwa na shtaka la kukutwa akipima korosho za wakulima kwa kutumia mawe bandia.

Akiwasomea mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Jaluyemba, mwendesha mashitaka mkaguzi msaidizi wa Polisi, Inspekta Bosco Kilumbe alidai kuwa,  watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti walinaswa wakiwa wananunua korosho kutoka kwa wakulima kinyume cha na utaratibu wa ununuzi wa zao hilo ambao hutolewa na Bodi ya Korosho Tanzania.

Inspekta Kilumbe alidai kuwa, katika matukio hayo, watuhumiwa walifanya kosa kinyume na kifungu namba 15 kifungu kidogo namba (4) cha Sheria ya Ununuzi wa Korosho namba 18 ya mwaka 2009.

Watuhumiwa wote walikana kufanya mashtaka hayo na hakimu alisema dhamana zao ziko wazi kwa atakayetimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye barua kutoka kwa mtendaji wa kijiji wakiwa na viambatanisho vya vitambulisho vya mpigakura.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 22, mwaka huu, kwa kutajwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad