Watu 15 Wakamatwa Akiwemo Daktari Aliyekamatwa na Gari la Wizara ya Afya Lililoibwa


Daktari Yusuf Mwaipopo(42) wa hospitali ya Ephraem ya Temeke jijini Dar amekamatwa kwa kukutwa na gari hilo katika maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro

Kaimu Kamanda wa Polisi Dar, DCP Liberat Sabas ametoa wito kwa madereva wa magari ya Umma kulaza magari kwenye ofisi za Serikali zenye usalama wa kutosha

Aidha, amesema magari mengine matano yaliyoibiwa yamekamatwa pamoja na bajaji na pikipiki. Pia silaha mbili, shot-gun yenye risasi nne na bastola yenye risasi nne

Alipoulizwa suala la Mashoga lilipofikia, amesema aulizwe aliyeanzisha Kampeni hiyo hawezi kutolea ufafanuzi kwa kuwa si yeye

Pia, alipoulizwa kuhusu kesi ya Wema Sepetu na kwanini amekamatwa mwenyewe, amesema kila aliyehusika atakamatwa na kufikishwa Mahakamani

Kusuhu sakata la kutekwa Mohammed Dewji amesema Polisi itakapokuwa na taarifa za kueleza Umma itaita Wanahabari na kueleza, upelelezi ni mchakato unaochukua muda
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad