Watu 37 Wafariki Kwenye Mapigano Kati ya Waislamu na Wakristo


Umoja wa Mataifa(UN) umetoa taarifa hiyo jana Novemba 16 na kueleza kuwa mapigano hayo yalisababisha Kanisa kuchomwa moto, watu zaidi ya 2,000 kuathirika na maelfu kukimbia makazi yao huko Alindao, Afrika ya Kati
-
Vyanzo vya habari vya Kanisa vimesema awali Mchungaji aliuliwa katika mapigano ya Alhamis baada ya Wapiganaji wa Kikristo maarufu 'Anti-Balaka' walipowaua Waislamu na kuibua mashambulizi ya kulipa kisasi
-
Najat Rochdi kutoka UN anayehusika na masuala ya Kibinadamu nchini humo alisema "Mashambulizi ya kila mara kwa raia hayakubaliki. Raia wanahitaji ulinzi, usalama na maisha mazuri ya baadaye"
-
Afrika ya Kati, moja ya nchi masikini ingawa ina utajiri wa dhahabu na Uranium imeshindwa kusimama tangu kutokea kwa vita vya wenye kwa wenye mwaka 2013 alipotolewa madarakani Rais Francois Bozize(Mkristo) na Waasi wa Kiislamu maarufu Seleka
-
Katika kuitikia hilo Wakristo ambao ni takribani asilimia 80 ya Watu nchini humo waliunda Kikundi cha kulipa kisasa kilichoitwa 'Anti-Balaka - #regrann

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad